KLABU ya Liverpool imefanikiwa kufikia dau la paundi milioni 32.5 kwa mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke hivyo kujiwekea mazingira mazuri ya kumsajili. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao 12 katika mechi 12 msimu uliopita na kuisaidia Villa kubakia katika Ligi Kuu. Liverpool wamefanikiwa kufikia kiwango hicho kilichohitajika na Villa baada ya kupokea fedha kutokana na mauzo ya Raheem Sterling aliyekwenda City kwa kitita cha paundi milioni 49. Pamoja na kutakiwa Livepool, Benteke bado ana mkataba na Villa ambao unamalika mwaka 2017. Benteke alijiunga na Aston Villa akitokea Genk Agosti mwaka 2012 kwa kitita cha paundi milioni saba na kufanikiwa kufunga mabao 49 katika mechi 101 alizocheza.
No comments:
Post a Comment