MENEJA wa Real Madrid, Rafael Benitez amesisitiza Sergio Ramos hataondoka katika klabu hiyo huku akimpamba beki huyo wa kati kama mchezaji muhimu katika kikosi chake. Manchester United wamekuwa wakijaribu kutaka kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 29 baada ya mazungumzo yake kuhusu mkataba mpya kukwama huku ule wa sasa ukitarajiwa kumalika Juni 2017. Hata hivyo, Benitez amesisitiza kuwa Madrid hawana mpango wowote wa kumuuza Ramos huku wakimjumuisha nyota huyo wa kimataifa wa Hispania katika kikosi chao kilichoanza ziara huko Australia. Akihojiwa Benitez amesema kuna taarifa nyingi zinazoendelea kuhusu Ramos, ila kwake yeye anadhani ni mchezaji makini ambaye bado mchango wake unahitajika Madrid. Benitez aliendelea kudai kuwa kuhusu taarifa za kuondoka anadhani hazina ukweli kwasababu rais Florentino Perez tayari alishaweka wazi kuwa hatamuuza.
No comments:
Post a Comment