SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA lina mpango wa kuzifanyia marekebisho kanuni zake ili kuzibana nchi zinazowania kuandaa Kombe la Dunia, zisitumie mwanya wa misaada ya kifedha kwa nchi nyingine kama rushwa. Kipengele kile kinachoziruhusu nchi zinazoshindania nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia kusambaza pesa katika nchi nyingine huenda kikafutwa. Aidha FIFA inazitaka nchi zote zinazowania nafasi hiyo kuzingatia haki za binadamu na sheria za kazi wakati wote. Hivi sasa nchi zinazotupiwa jicho ni Urusi inayoandaa Kombe la Dunia mwaka 2018 na Qatar inayoandaa 2022. Kura za kuamua nchi gani italiandaa Kombe la Dunia la mwaka 2026 zitapigwa mwaka 2017 huko Kuala Lumpur, Malaysia. Nchi zinazoiwania nafasi hiyo ni Marekani, Canada, Mexico na Colombia.
No comments:
Post a Comment