Saturday, July 4, 2015

MAN CITY YATENGA PAUNDI MILIONI 100 KWA AJILI YA KUWANASA KINA POGBA, DE BRUYNE NA STERLING.

KLABU ya Manchester City inatarajia kutumia paundi milioni 100 kwa ajili ya usajili wa wachezaji wapya msimu huu baada ya vikwazo walivyowekewa kuhusu ununuzi wa wachezaji kuondolewa na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA. City ilipigwa faini ya paundi milioni 49 na kulazimishwa kutoa kikosi chenye upungufu wa wachezaji 21 msimu uliopita baada ya kukiuka sheria za matumizi ya fedha za UEFA. Lakini baada ya kutimiza masharti hayo, timu hiyo sasa iko huru kuwasaka wachezaji wapya akiwemo Paul Pogba, Kevin De Bruyne na Raheem Sterling. Ununuzi wa mchezaji wa Aston Villa Fabian Delph atakayegharimu paundi milioni 8 pia unatiliwa maanani, huku Barcelona ikiongoza harakati za kutaka kumsajili Pogba. Lakini licha ya kupewa ruhusa ya kufanya matumizi inavyotaka katika dirisha la uhamisho,City imeonywa kwamba fedha zake zitaendelea kuchunguzwa ili kuhakikisha kuwa inaafikia masharti makali yaliowekwa.

No comments:

Post a Comment