KLABU ya Galatasaray imedai kuwa mshambuliaji Lukas Podolski ameikacha Arsenal na kujiunga nao. Mabingwa hao wa Uturuki wamesema nyota huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 30 anatarajiwa kukamilisha usajili wake leo baada ya kufanyiwa vipimo vya afya. Podolski alihamia Arsenal akitokea klabu ya FC Koln ya Ujerumani mwaka 2012 kwa kitita cha paundi milioni 11 na kufanikiwa kufunga mabao 31 katika mechi 82 alizoichezea Gunners. Nyota huyo aliisaidia Arsenal kushinda taji la FA mwaka 2013 lakini mzunguko wa pili wa msimu uliopita alipelekwa kwa mkopo Inter Milan ya Italia. Nafasi ya Podolski ilizidi kuwa finyu baada ya meneja Arsene Wenger kuwaongeza Mesut Ozil, Alexis Sanchez na Danny Welbeck katika safu ya ushambuliaji huku pia akiwa na kina Theo Walcott, Olivier Giroud na Alex Oxlade-Chamberlain.
No comments:
Post a Comment