Saturday, July 4, 2015

MWILI WA EUSEBIO WAZIKWA RASMI KATIKA ENEO LA WATU MAARUFU.

MWILI wa mwanasoka nguli Eusebio umezikwa rasmi katika kanisa kuu nchini Ureno ikiwa kama heshima ya mwisho kwa mwanasoka huyo shujaa. Mwili wa nguli huyo aliyekuwa akijulikana kama Black Panther, ambaye alifariki dunia Januari mwaka jana akiwa na umri wa miaka 71, ulipitishwa juu farasi kuzunguka jijini la Lisbon pamoja na Uwanja wa Benfica kabla ya kuenda kupumzishwa katika nyumba yake ya milele. Serikali ya Ureno ilitoa siku tatu za maombolezo baada ya kifo cha mmoja kati ya washambuliaji waliokuwa wakiogopewa sana duniani huku mapema mwaka huu zikipigwa kura kwa Eusebio sa Silva Ferreira kuzikwa katika eneo hilo ambalo ni maalumu kwa wa wanasiasa na watu wengine maarufu. Maelfu ya watu walijitokeza katika mitaa ya Lisbon siku ya mazishi yake mwaka jana kutoa heshima zao nguli huyo ambaye ndiye mchezaji wa kwanza mweusi kutunukiwa tuzo ya Ballon d’Or mwaka 1965. Eusebio mzaliwa wa Msumbiji ambalo ni koloni la zamani la Ureno, alihamia Benfica akiwa na umri wa miaka 19 na kuwa mchezaji muhimu aliyeisaidia timu hiyo kunyakuwa Kombe la Ulaya mwaka 1962 huku akifunga mabao mawili katika mchezo wa fainali walioshinda mabao 5-3 dhidi ya Real Madrid. Eusebio pia aliwahi kunyakuwa mataji 11 ya Ligi Kuu ya Ureno na matano ya Kombe la Ligi katika kipindi cha miaka 15 ambayo amekuwa akiitumikia Benfica na kufunga mabao 733 katika mechi 745.

No comments:

Post a Comment