BEKI wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Cafu anaamini taifa hilo limekuwa haliogopewi tena na wapinzani wao baada ya kutolewa nje katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Copa America. Brazil walitolewa katika michuano hiyo ya nchi za bara la Amerika Kusini kwa matuta na Paraguay ikiwa imepita mwaka mmoja baada ya kusasambuliwa mabao 7-1 katika ardhi yao na mabingwa wa Kombe la Dunia Brazil. Cafu ambaye amewahi kushinda mataji mawili ya Kombe la Dunia na Copa America katika kipindi cha miaka 16 aliyocheza soka anaamini vipigo hivyo sio vimeondoa hali ya kujiamini kwa wachezaji lakini pia kutoogopewa tena katika soka na mataifa mengine duniani. Cafu amesema Brazil wamekosa ari na moyo wa kujituma katika soka na sasa wanacheza na wapinzani ambao hawaahofii tena kama ilivyokuwa zamani. Hata hivyo, Cafu aliendelea kudai kuwa Brazil inapita katika kipindi cha mpito kwasasa lakini watakuja tena kutawala soka na kuwafanya wapinzani kuwahofia tena huku wale wanaowaponda wakishangazwa na mabadiliko hayo.
No comments:
Post a Comment