MKURUGENZI wa michezo wa AS Roma, Walter Sabatini amethibitisha kuwa klabu hiyo inajaribu kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 ni mmoja ya wachezaji ambao City inataka kuwaacha katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, ingawa Dzeko mwenye amedai hatalazimisha kuondoka. Akihojiwa Sabatini amesema pamoja na kuwa hawako karibu kumsajili lakini Roma itafanya kila iwezalo kuhakikisha wanapata saini yake kiangazi hiki. Sabatini aliendelea kudai kuwa anadhani Dzeko atakuwa mchezaji sahihi katika kikosi chao ingawa amekiri kuwa atawagharimu kama wakifanikiwa.
No comments:
Post a Comment