MKURUGENZI wa michezo wa Bayern Munich, Matthias Sammer amewakosoa watu wanaodai kuwa Douglas Costa ni mbadala wa Franck Ribery, akidai kuwa wanakosa heshima. Costa alikamilisha uhamisho wake wa kitita cha euro milioni 30 kwenda Bayern jana, akisaini mkataba wa miaka mitano kutokea klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa Ujerumani lakini Sammer amepuuza taarifa kuwa Costa ameletwa ili kuziba nafasi ya Ribery mwenye umri wa miaka 32 ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya muda mrefu. Akihojiwa Sammer amesema pamoja na kwamba Costa ana uwezo wa kucheza nafasi tofauti katika safu ya ushambuliaji ikiwemo ya winga haimaanishi kuwa ndio mbadala wa Ribery. Sammer aliendelea kudai kuwa Ribery kwasasa ni majeruhi lakini bado ataendelea kuwa mchezaji wao na wako pamoja naye kwa kila kitu mpaka hapo ataaporejea katika afya yake.
No comments:
Post a Comment