MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Neymar amesema picha za video zilizomuonyesha akiwa amelewa katika sherehe nyumbani kwake zinaonyesha ukweli kuwa hawezi kupumzika akiwa nchini kwao Brazil. Katika picha hizo Neymar ambaye pia ni nahodha wa Brazil alionekana kuwa hoi mwishoni mwa sherehe hiyo aliyokuwa na marafiki zake akiwemo mchezaji mwenzake wa zamani wa Santos, Ganso. Neymar mwenye umri wa miaka 23 amekosolewa vikali kwa tabia yake hiyo na baadhi ya wachambuzi ambao bado wana hasira na ukweli kuwa mshambuliaji alifungiwa mechi nne kwa kosa alilojisababishia katika mchezo wa michuano ya Copa America dhidi ya Colombia mwezi uliopita. Hata hivyo, Neymar amefafanua kiurahisi kuwa hawezi kupata muda binafsi wakati akirejea Brazil. Neymar aliwaambia wana habari kuwa ilikuwa bahati mbaya kumualika mtu ambaye alikuwa hamhusu kwani alikuwa likizo na marafiki zake na tukio hilo likatokea.
No comments:
Post a Comment