BEKI wa kimataifa wa Brazil, Dani Alves amesema meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola anataka kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo. Alves anayecheza katika klabu ya Barcelona amesema meneja wake huyo wa zamani ana mipango ya kuwafanya Brazil mabingwa tena. Lakini Alves amedai kuwa maofisa wa soka wa Brazil wanaogopa kuajiri kocha wa kigeni kwa ajili ya timu yao ya taifa. Akihojiwa na luninga ya ESPN, Alves amesema Pep alimwambia anataka kuinoa Brazil na kuwafanya kuwa mabingwa tena lakini hadhani hilo litawezekana kwa nchi hiyo kukubali kunolewa kocha mgeni. Chini Guardiola, Barcelona walijiimarisha na kutawala soka la vilabu kwa kushinda mataji 14 katika misimu minne yakiwemo mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Guardiola aliondoka Barcelona Juni mwaka 2012 na kuchaguliwa kuinoa Bayern majira ya kiangazi yaliyofuata ambapo ameisaidia klabu hiyo kunyakuwa taji la pili mfululizo la Bundesliga.
No comments:
Post a Comment