KOCHA wa timu ya taifa ya Italia, Antonio Conte anaweza kukabiliwa na mshtaka ya jinai kuhusiana na tuhuma za kuhusika kwake na upangaji wa matokeo katika mechi mwaka 2011. Kocha huyo tayari ameshatumikia adhabu kwa kutotoa taarifa za upangwaji matokeo katika mechi mbili za klabu yake ya zamani ya Siena katika msimu wa 2010-2011. Kocha huyo wa zamani wa Juventus ni miongoni mwa watu 104 ambao mwendesha mashitaka ametaka washitakiwe kutokana na sakata hilo. Hata hivyo, Conte mwenye umri wa miaka 45 mara zote amekuwa akikanusha kuwa kutenda makosa hayo. Kabla ya kuanza kuinoa Italia mwaka jana, Conte alitokea Juventus ambapo aliisaidia timu hiyo kunyakuwa mataji matatu mfululizo ya Serie A.
No comments:
Post a Comment