Wednesday, July 8, 2015

AL AIN YAMCHUKUA EMENIKE KWA MKOPO KUZIBA NAFASI YA GYAN.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Nigeria, Emmanuel Emenike anatarajiwa kuhamia kwa mkopo katika klabu ya Al Ain ya Muungano wa Falme za Kiarabu-UAE kuchukua nafasi ya nyota wa kimataifa wa Ghana Asamoah Gyan ambaye ametimikia nchini China. Al Ain ilikuwa ofa kutoka klabu ya Shanghai SIPG ambayo inanolewa na kocha wa zamani wa timu ya taifa Uingereza Sven-Goran Eriksson. Gyan mwenye umri wa miaka 29 amewasili China mapema leo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili wake katika klabu hiyo. Emenike yeye anatarajiwa kuwasili UAE kesho kwa ajili ya kukamilisha taratibu zake za mkopo akitokea klabu ya Fenerbahce ya Uturuki. Katika dili hilo la mkopo kutakuwa na kipengele kinachowapa nafasi Al Ain kumnunua moja kwa moja Emenike kama watavutiwa naye.

No comments:

Post a Comment