MSHAMBULIAJI mpya wa Manchester City, Raheem Sterling amesema anashukuru kukamilisha uhamisho wake kutoka Liverpool uliogharimu paundi milioni 49 na yuko tayari kupambana na changamoto mpya. Winga huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20, anaamini kuwa ataimarika kama mchezaji akiwa Etihad baada ya kuwa mchezaji ghali kuwahi kutokea nchini Uingereza. Akihojiwa Sterling amesema anashukuru kila kimekwisha sasa na anaamini kutokana na ubora wa wachezaji waliopo City haitamuwia kazi kubwa kuimarisha na kuwa bora zaidi.
Sterling katika na mkataba na Liverpool mpaka mwaka 2017 lakini alikataa ofa ya kuongeza mkataba mwingine wa miaka mitano ambao ungemuwezesha kulipwa paundi 100,000 kwa wiki. Nyota huyo tayari asubuhi leo amechukua ndege kwenda Australia kujiunga na wachezaji wenzake wa Manchester City waliopo katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya. Sterling amepewa mkataba wa miaka mitano City ambao utamuwezesha kulipwa kitita cha paundi 180,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment