Monday, July 27, 2015

VAN GAAL ADOKEZA ROMERO ANAWEZA KUWA MBADALA WA DE GEA.

MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amedokeza kuwa wamemsajili golikipa Sergio Romero (pichani) ili kujiandaa na uwezekano wa kuondoka kwa David de Gea katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Romero alikamilisha uhamisho wake kutua Old Trafford baada ya kukubali kusaini mkataba wa miaka mitatu huku akiwa na nafasi ya kuongezwa mwingine. De Gea amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Real Madrid baada ya kuondoka kwa Iker Casillas. Kufuatia Victor Valdes kujiandaa kuondoka baada ya kukataa kucheza katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 msimu uliopita, Van Gaal ana Romero atakuwa chaguo sahihi hata kama De Gea naye ataamua kuondoka United. Akihojiwa Van Gaal amesema hajui kama De Gea ataondoka au atabakia hivyo ni vyema kwao kujiandaa na lolote na anadhani Romero atakuwa chaguo sahihi.

No comments:

Post a Comment