KIUNGO wa Juventus, Arturo Vidal amefungiwa kuendesha gari kwa muda wa miaka miwili baada ya kubambwa akiendesha huku amekunywa pombe wakati wa michuano ya Copa America ambayo Chile waliibuka washindi. Vidal mwenye umri wa miaka 28 alipata ajali na gari lake la kifahari aina ya Ferrari Juni 17 mwaka huu lakini alitoka salama huku mkewe akipata majeraha madogo katika mkono wake. Pamoja na kushitakiwa kwa kuendesha huku akiwa amelewa, Vidal aliweza kuendelea kuitumikia Chile kwa mechi zote za michuano hiyo. Mbali na kufungiwa leseni yake, Vidal pia ametakiwa kufanya shughuli za kijamii katika eneo ambalo kulitokea ajali hiyo. Kiungo huyo pia aliwatukana polisi wawili waliokuwepo eneo la tukio hivyo kutakiwa kuwaomba radhi pamoja na jamii yote inayozunguka eneo hilo.
No comments:
Post a Comment