Thursday, July 9, 2015

WENGER AWATEMA NYOTA KADHAA KATIKA KIKOSI CHAKE.

WACHEZAJI nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez, Danny Welbeck na Tomas Rosicky ni miongoni mwa wachezaji walioachwa katika kikosi cha timu hiyo kitakachoshiriki michuano ya mifupi kugombea taji la Asia. Sanchez na golikipa wa kimataifa wa Colombia wote wanakosa kufuatia ushiriki wao wa michuano ya Copa America ambayo Chile ndio walioibuka washindi wakati Welbeck na Rosicky wenyewe wameachwa katika michuano hiyo ya kirafiki itakayoanza Julai 15 mpaka 18 kutokana na majeruhi. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alikaririwa katika matandao akidai kuwa Calum Chembers ameamua kufupisha likizo yake na kurudi kikosini kesho huku Welbeck na Rosicky wakiwa hawajapona majeruhi yao waliyopata mwishoni mwa msimu uliopita. Kwa upande wa Ospina, Wenger amesema amepewa likizo mpaka Julai 27 huku Sanchez yeye akipewa mpaka Agosti 3 baada ya nchi yake kuibuka kidedea katika Copa America.

No comments:

Post a Comment