Thursday, July 9, 2015

BABU AMTUHUMU MESSI KWA UVIVU.

BABU yake Lionel Messi, Antonio Cuccitini amesema mjukuu wake huyo alikuwa mvivu katika hatua za mwisho za michuano ya Copa America iliyomalizika hivi karibuni nchini Chile. Nahodha huyo wa Argentina alifunga bao moja pekee katika michuano hiyo wakati walipotandikwa na wenyeji Chile kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika mchezo wa fainali uliofanyika Jumamosi iliyopita. Babu yake Messi anaamini kuwa mjukuu wake huyo angeweza kufanya mengi zaidi kuisaidia nchi yake kunyakuwa taji lake la kwanza baada ya kupita miaka zaidi ya 20. Akihojiwa Cuccitini amesema mwanzoni Messi alikuwa mchezoni lakini katika mechi tatu za mwisho hakuwa yule tena waliomzoea kwani alikuwa mvivu.

No comments:

Post a Comment