SHIRIKISHO la Soka la Amerika Kaskazini, Kati na Caribbean-Concacaf limethibitisha jana kumteua mwanamama Sonia Bien-Aime kutoka Turks na Caicos kuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka la Duniani-FIFA. Bien-Aime ambaye anawakilisha eneo la Caribbean, anakuwa mwanamke wa pili kuwa mjumbe wa kamati hiyo baada ya Lydia Nsekera wa Burundi naye kuwahi kushikilia wadhifa huo. Mwanamama huyo anachukua nafasi ya Jeffrey Webb rais wa Concacaf aliyesimamishwa, kama mwakilishi wa Caribbean. Webb kwasas amezuiwa nchini Uswisi baada ya kuhusishwa na masuala ya ufisadi katika uchunguzi unaosimamiwa na Marekani. Concacaf wana nafasi tatu za ujumbe wa kamati ya Utendaji ya FIFA hivyo makamu wa rais wa shirikisho hilo Alfredo Hawit anakuwa mwakilishi kutoka America ya Kati na rais wa Shirikisho la Soka la Marekani Sunil Gulati anayewakilisha Amerika Kaskazini ataendelea na nafasi yake hiyo.
No comments:
Post a Comment