Monday, July 27, 2015

WALCOTT NJIANI KUSAINI MKATABA MPYA ARSENAL.

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Theo Walcott anakaribia kuongeza mkataba wake na klabu hiyo hadi mwaka wa 2019. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amefichua kuwa Walcott atasaini mkataba mpya na timu hiyo huku ule wake wa awali ukiwa umebaki mwaka mmoja. Walcott mwenye umri wa miaka 26 aliifungia Arsenal goli la kipekee dhidi ya Wolfsburg ya Ujerumani na kuiwezesha timu hiyo kunyakuwa Kombe la Emirates jana. Aidha, kipa wa Poland, Scszesny yuko mjini Roma, Italia akimalizia taratibu za mwisho za kujiunga na klabu ya AS Roma baada ya kupoteza nafasi yake kwa aliyekuwa kipa wa Chelsea, Petr Cech. Scszesny kwasasa anasubiri vipimo vya afya kabla ya kujiunga na timu hiyo kwa mkopo. Wenger, amekuwa chini ya shinikizo kali kuimarisha kikosi chake ili kuleta ushindani katika Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment