Monday, July 27, 2015

VAN GAAL KUONDOKA UNITED KWA AJILI MKEWE.

MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal pengine akaondoka klabuni hapo mwishoni mwa mkataba wake wa miaka mitatu ili kutimiza ahadi aliyompa mkewe. Akiulizwa kuhusu kuongeza mkataba Old Trafford, Van Gaal raia wa Uholanzi alidai kuwa ameamua kuondoka pindi atakapomaliza mkataba wake. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63, amesema sababu inayoweza kumfanya aondoke ni ahadi aliyompa mkewe kwakuwa hawajapa muda wa kutosha kukaa pamoja. Van Gaal amesema alimuahidi mkewe Truus kuwa atakapofikisha umri wa miaka 55 atastaafu lakini mpaka sasa bado anafanya kazi na wiki ijayo anatimiza umri wa miaka 64. Van Gaal aliendelea kudai kuwa ndoto yake kubwa ilikuwa kufundisha katika Ligi Kuu pia hivyo haoni sababu ya kuendelea pindi atakapomaliza mkataba wake.

No comments:

Post a Comment