Monday, July 27, 2015

AL-ITTIHAD KUWAKUTANISHA WATUKUTU WA GHANA, MUNTARI NA BOATENG.

KLABU kongwe ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia inaweza kuwakutanisha nyota wa zamani wa AC Milan ya Italia Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng katika timu hiyo. Wawili hao ambao walisimamishwa kuitumikia timu ya taifa ya Ghana kutokana na sababu tofauti za utovu wa nidhamu wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014, walikuwa kwa pamoja wakiitumikia Milan mismu mitatu iliyopita kabla ya Boateng hajahamia Schalke ya ujerumani. Muntari na Boateng ambao wanajulikana kwa urafiki wao, kwasasa wako sokoni katika kipindi hiki cha usajili wa kiangazi. Muntari mwenye umri wa miaka 30, ni mchezaji huru baada ya kusitisha mkataba wake na Milan na tayari inaripotiwa kuwa ameshakubali kusaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya euro milioni 2.5 kila mwaka na Ittihad. Klabu hiyo pia imeripotiwa kumuwinda Boateng baada ya kushindwa kumsajili kiungo Fredy Guarin kutoka Inter Milan.

No comments:

Post a Comment