Monday, July 27, 2015

LUIZ AMPIGIA DEBE DI MARIA KWENDA PSG.

KIUNGO wa Paris Saint-Germain-PSG, David Luiz ana matumaini ya kusajiliwa kwa Angel Di Maria, kwani anaamini ujio wake utawafanya kuwa wapinzani wa kweli katika kugombea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Inadaiwa kuwa kiungo huo mwenye umri wa miaka 27 anakaribia kufanya uhamisho wake kutoka Manchester United kwenda PSG baada ya kushindwa kujiunga na kikosi cha United katika ziara yao nchini Marekani huku meneja wa PSG Laurent Blanc akikiri kuwepo kwa uwezekano huo. Di Maria amekuwa akihangaika kucheza kwa kiwango chake toka asajiliwe kwa kitita kilichovunja rekodi nchini Uingereza cha paundi milioni 59.7 na United mwaka jana. Lakini Luiz ana uhakika kuwa Di Maria bado ni mchezaji mwenye ubora ambaye anaweza kuisaidia PSG kutawala soka la Ulaya kama akisajiliwa. Luiz amesema wanataka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Di Maria ni mchezaji anayeweza kuwasaidia kuvuka hatua nyingine.

No comments:

Post a Comment