TIMU ya taifa ya Mexico imefanikiwa kuweka rekodi kwa kunyakuwa Kombe la Gold kwa mara ya saba baada ya kuichapa Jamaica walioingia kwa mara ya kwanza katika fainali ya michuano hiyo. Jamaica imekuwa nchi ya kwanza kutoka ukanda wa Caribbean kutwaa taji hilo lakini walishindwa kufurukuta mbele ya Mexico ambao hilo ni tatu lao la tatu katika fainali nne zilizopita za michuano hiyo. Katika mchezo huo Mexico walifanikiwa kushinda mabao 3-1 mbele ya mashabiki 70,000 waliojitokeza katika Uwanja wa Philadelphia Lincoln ambayo yalifungwa na Andres Guardado, Jesus Corona na Oribe peralta huku lile la kufutia machozi kwa upande wa Jamaica likifungwa na Darren Mattocks. Akihojiwa mara baada ya fainali ya michuano hiyo ambayop hushirikisha nchi za ukanda wa Amerika Kaskazini, Kati na Caribbean-Concacaf, Kocha wa Mexico Miguel Herrera amesema hiyo ni siku ya kipekee kwao. Mexico sasa wamefuzu kwa ajili ya hatua ya mtoano dhidi ya mabingwa wa mwaka 2013 Marekani mchezo ambao utachezwa Octoba 9 mwaka huu katika kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho nchini Urusi mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment