RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amepuuza tetesi zinazomuhusisha Neymar na klabu ya Manchester United na kubainisha kuwa wanataka nyota huyo wa kimataifa wa Brazil astaafu akiwa Camp Nou. Kumekuwa tetesi hivi karibuni zikidai kuwa United wanajipanga kuvunja rekodi kwa kuwania kumsajili Neymar kabla dirisha la usajili halijafungwa huku baadhi ya vyombo vya habari vikidai pia nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 yuko tayari kutua Old Trafford. Hata hivyo, Bartomeu amekanusha taarifa hizo akidai kuwa Barcelona hawana mpango wowote wa kuuza mmmoja kati ya wachezaji muhimu na kufafanua kuwa wana matumaini mazuri ya hivi karibuni kusaini naye mkataba mwingine mrefu zaidi. Bartomeu amesema hawataki Neymar aondoke kwani bado mdogo na wanataka astaafu akiwa hapo. Rais huyo aliendelea kudai kuwa wataanza mazungumzo naye ya mkataba mpya katika kipindi cha miezi michache ijayo kwa ajili ya kumuongeza mkataba mrefu zaidi.
No comments:
Post a Comment