WINGA mahiri wa kimataifa wa Argentina, Angela Di Maria amekiri mambo hayakumuendea vyema katika klabu ya Manchester United kufuatia kukamilisha uhamisho wake kwenda Paris Saint-Germain-PSG uliogharimu kitita cha paundi milioni 44.3. Di Maria mwenye umri wa miaka 27 amebainisha kuwa familia yake haikuwa na furaha ya kuishi jijini Manchester kufuatia kuvamiwa na majambazi nyumbani kwake Cheshire. Akihojiwa Di Maria amesema kwasasa ana furaha kwasababu anajua mke na mtoto wake watakuwa na furaha ya kuishi katika jiji la Paris. Nyota huyo aliongeza kuwa haukuwa uamuzi wake kuondoka kwani pande zote tatu zilikubaliana wakiwemo United ambao waliridhia kumuuza. Di Maria alijiunga na United akitokea Real Madrid kiangazi mwaka jana kwa kitita kilichovunja rekodi ya usajili nchini Uingereza cha paundi milioni 59.7.
No comments:
Post a Comment