RAIS wa klabu ya Lyon, Jean-Michel Aulas amedai kuwa timu hiyo inajipanga kukamilisha uhamisho wa beki wa kulia wa Manchester United Rafael. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 25, alichezeshwa mara 11 pekee chini ya meneja Louis van Gaal msimu uliopita na hakujumuishwa katika kikosi cha United kilichofanya ziara nchini Marekani mwezi uliopita. Rafael sasa amesafiri kuelekea nchini Ufaransa ili kukamilisha uhamisho wake Lyon na Aulas alithibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter. Julai mwaka huu wakala wa Rafael alidai kuwa United ilikuwa tayari kumtoa beki huyo kwa klabu ya Benfica ili waweze kumnasa Nicolas Gaitan..
No comments:
Post a Comment