Monday, August 3, 2015

WENGER AANZA KUTAMBA BAADA YA KUIBANJUA CHELSEA.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini wachezaji wake wamefanikiwa kuvuka kikwazo kikubwa cha kiakili kwa kuifunga Chelsea katika mchezo wa Ngao ya Hisani jana. Arsenal walikuwa hawajawahi kuifunga Chelsea chini ya Jose Mourinho katika mechi 13 walizokutakana kabla ya mchezo wa jana. Lakini bao la Alex Oxlade-Chamberlain lilitosha kuipa ushindi Arsenal wa bao 1-0 dhidi ya mabingwa hao wa Ligi Kuu katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Wembley. Akihojiwa Wenger amesema ilikuwa muhimu kwa kikosi chake kukiondoa kikwazo hicho mbele yao hivyo ana imani ari ya ushindi itakuwa imeongezeka kuelekea katika msimu mpya.

No comments:

Post a Comment