Monday, August 3, 2015

SAFARI YA MESSI GABON YAZIDI KUZUA MAZITO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi ameshutumiwa na Shirika la Haki za Binadamu, ambao wamemtuhumu kuungana na wakandamizaji katika ziara yake ya Gabon hivi karibuni. Messi alipigwa picha akiwa na rais wa Gabon Ali Bongo ambaye anatajwa kama diktekta, baada ya kusaidia kuweka jiwe la msingi katika uwanja mpya utakaotumika kwa ajili ya fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2017. Mbali na kuweka jiwe hilo la msingi, Messi alitembelea kituo cha afya kinachoendeshwa na serikali ya nchi hiyo pamoja na mgahawa unaomilikiwa na familia ya Bongo. Wakati serikali ya Gabon ikikanusha taarifa kuwa Messi alilipwa mamilioni ya fedha kwenda nchini humo mwezi uliopita, sasa nay eye mwenyewe amekuwa akikosolewa vikali kwa kuonekana hadharani akiunga mkono utawala wa Bongo. Rais huyo amekuwa akituhumiwa na masuala ya ufisadi huko nyuma pamoja na kukiuka haki za binadamu ikiwemo kuzia uchunguzi wa mauaji ya watoto yanayodaiwa kuelendelea nchini humo.

No comments:

Post a Comment