MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amemkingia kifua kiungo wake Francis Coquelin akidai kuwa amekuwa akifanya kazi kubwa akiwa kama chaguo namba moja katika nafasi ya kiungo mkabaji. Beki wa zamani wa Manchester United ambaye kwasasa ni mchambuzi Gary Neville aliponda nafasi ya kiungo ya Arsenal haswa Coquelin lakini Wenger anaonekana kuwa na imani na nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24. Wenger aliuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa Coquelin ana rekodi nzuri katika nafasi ya ulinzi na amekuwa akifanya kazi nzuri toka kuanza kwa msimu huu. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 aliendelea kudai kuwa kama watu watakuwa wanatizama soka kama anavyotizama yeye anadhani wataona kazi nzuri anayofanya.
No comments:
Post a Comment