MSHAMBULIAJI wa Chelsea Diego Costa ameshtakiwa kwa madai ya kutaka kuzua ghasia ambayo haikuonekana na mwamuzi lakini ambayo yimenaswa katika picha za video.Mshambuliaji huyo anahusishwa katika tukio la kumfanyia vurugu beki wa Arsenal Laurent Koscielny katika dakika ya 43 ya mechi.Naye Beki wa Arsenal Gabriel ameshtakiwa kwa utovu wa nidhamu kwa tabia yake wakati alipopewa kadi nyekundu huku Santi Carzola akionywa kuhusu tabia yake mbaya.Wakati huohuo vilabu vyote viwili vimeshtakiwa kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake chini ya sheria za FA.Vilabu vyote viwili, Costa na Gabriel anatakiwa kujibu mashitaka hayo mpaka kesho jioni.
No comments:
Post a Comment