NGULI wa zamani wa soka wa Ujerumani, Dietmar Hamann amesema angempa Pep Guardiola maksi tano kwa kumi katika msimu miwili ambayo ameingoza Bayern Munich na anaamini klabu hiyo inapaswa kutafuta kocha mwingine. Guardiola ambaye alikuwa kocha wa barcelona kabla ya kutua Munich, ameisaidia timu hiyo kushinda mataji mawili ya Bundesliga lakini ameshindwa kufanikiwa barani Ulaya baada ya kutolewa mara mbili katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Bayern pia walitolewa katika nusu fainali ya DFB Pokal msimu uliopita kwa kutandikwa na Borussia Dortmund kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Akihojiwa Hamann amesema anaamini klabu haitakuwa vibaya kama wakileta kocha mwingine kwani Guardiola ameshindwa kuleta mafanikio yaliyotegemewa kwa kipindi cha msimu miwili alichokuwepo hapo. Hamann aliendelea kudai kuwa Bayern wamekuwa vizuri kwenye ligi lakini sehemu nyingine wamekuwa wakivurunda jambo ambalo hadhani kama enzi za kina Louis van Gaal na Jupp Heynckes wangevumiliwa.
No comments:
Post a Comment