Friday, September 11, 2015

HATIMAYE MAN UNITED YAFANIKIWA KUMPIGA PINI DE GEA.

GOLIKIPA wa Manchester United, David de Gea amesaini mkataba mpya wa miaka minne na klabu hiyo huku kukiwa na kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 24, ambaye alitua Old Trafford akitokea Atletico Madrid mwaka 2011 alikuwa akitegemewa kurejea La Liga kujiunga na Real Madrid kiangazi hiki. Hata hivyo, kufuatia uhamisho huo kushindikana katika siku ya mwisho kutokana na baadhi ya karatasi kuchelewa kufika, De Gea ameamua kusaini mkataba mwingine na klabu hiyo. Akihojiwa mara baada ya kusaini mkataba huo, De Gea amesema amefurahi kuanza ukurasa mpya katika maisha yake ya soka akiwa na United. Golikipa huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa anataka kuachana na wakati mgumu aliopata majira ya kiangazi na kuanza kujituma kwa bidii ili aweze aweze kuisaidia United kupata mafanikio.

No comments:

Post a Comment