MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho amethibitisha kuwa golikipa wake Thibaut Courtois anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa goti na anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23 alipata majeruhi hayo wakati akiwa mazoezini Jumatano iliyopita. Mourinho alithibitisha taarifa hizo kabla ya kusafiri kuifuata Everton kwa ajili ya mchezo wao wa kesho na kudai kuwa ni pigo kubwa kwa kikosi chake. Golikipa wa zamani wa Stoke City Asmir Begovic anatarajiwa kuchukua nafasi ya Courtois katika mchezo huo wa kesho. Baada ya mismu mitatu ya mkopo katika klabu ya Atletico Madrid, Courtois alichukuliwa kuwa kipa namba moja wa Chelsea katika msimu wa 2014-2015 akichukua nafasi ya Petr Cech.
Friday, September 11, 2015
CHELSEA MAJANGA, COURTOIS AHITAJI UPASUAJI.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment