MENEJA wa Barcelona, Luis Enrique amedai kuwa Lionel Messi yuko tayari kucheza mchezo wa kesho wa La Liga dhidi ya Atletico Madrid pamoja na kukosa mazoezi leo kutokana na sababu binafsi. Mshambuliaji huyo hajafanya mazoezi toka arejee kutoka katika majukumu ya kimataifa na Argentina lakini amejumuishwa katika kikosi kitakachopambana na Atletico kesho. Vyombo vya habari nchini Hispania vimeripoti kuwa Messi hajaonekana kutokana na kutingwa na majukumu ya kifamilia kufuatia mkewe kujifungua mtoto wao wa pili ingawa hakuna uthibitisho wowote kutoka kwa nyota huyo. Akizungumza na wana habari, Enrique amesema Messi ana ruhusa ya klabu ya kukosa mazoezi kutokana na sababu binafsi. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa pamoja na kukosekana huko lakini atakuwepo katika mchezo wa kesho dhidi ya Atletico.
No comments:
Post a Comment