MSHAMBULIAJI wa Manchester City, David Silva ameondolewa katika kikosi cha timu hiyo kitakachochuana na Crystal Palace Jumamosi hii kutokana na majeruhi ya kifundo cha mguu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 ameanza msimu katika kiwango bora akifunga bao moja na kusaidia mengine manne katika mechi nne za Ligi Kuu zilizochezwa. Akihojiwa meneja wa City, Manuel Pellegrini alithibitisha taarifa za kumuondoa Silva kikosi chake lakini amedai kuwa amefanya hivyo kwa tahadhari ili kuepusha kutoneshwa kabla hajapona. Pellegrini amesema ana matumaini makubwa ya kumtumia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus Jumanne ijayo.
No comments:
Post a Comment