Friday, September 4, 2015

LEONARDO AMPONDA NEYMAR.

MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Leonardo amesema ana mashaka kama Neymar ana sifa zinazohitajika kuwa kiongozi wa timu ya taifa ya nchi hiyo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 aliteuliwa nahodha katika kikosi cha Dunga baada ya Kombe la Dunia mwaka jana lakini amekuwa akikosolewa kufuatia tukio alilofanya katika michuano ya Copa America mapema kiangazi hiki. Neymar alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo wa hatua ya makundi waliofungwa na Colombia baada ya kumpiga kichwa Jeison Murillo na baadae kufungiwa mechi nne zaidi zilizomfanya kukosa kabisa michuano hiyo. Akihojiwa Leonardo amesema neymar ni mchezaji mkubwa lakini hadhani kama amekomaa sawasawa kuiongoza Brazil na kuibeba timu kwa mikono yake. Nyota huyo wa zamani aliendelea kudai kuwa pamoja na uwezo na kipaji alichonacho mchezaji huyo lakini anadhani wakati wa yeye kuwa nahodha bado kutokana na makosa ambayo amekuwa akifanya.

No comments:

Post a Comment