Friday, September 4, 2015

BAYERN KUSAIDIA WAKIMBIZI.

KLABU ya Bayern Munich inajipanga kuweka kambi ya mazoezi kwa ajili ya wakimbizi wanaomiminika nchini Ujerumani na wanatarajiwa kutoa msaada wa euro milioni moja kwa ajili ya kufadhili miradi ya wakimbizi hao. Baadhi ya nchi za Ulaya zimeshuhudia lundo la wahamiaji huku wengi wakiwa nchini Hungary wakitaka kusafiri kuelekea Ujerumani. Mabingwa hao wa bundesliga wamepanga kutoa vyakula, masomo ya kijerumani na vifaa vya soka kwa ajili ya watoto. Ofisa mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge amesema klabu hiyo inaona wana jukumu kama jamii kusadia wakimbizi hao. Idadi ya wakimbizi wanaoingia Ulaya imevunja rekodi mwaka huu, wengi wao wakiwa wanakimbia machafuko ya Syria huku Ujerumani ikitegemea kupokea wakimbizi zaidi ya 800,000 ikiwa ni mara nne ya wale waliopokewa mwaka jana.

No comments:

Post a Comment