Friday, September 4, 2015

PEREZ AIPONDA MAN UNITED.

RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez amefafanua kuwa usajili wa David de Gea ulishindikana kwasababu Manchester United walitumia saa nane kuwatumia karatasi muhimu zilizohitajika. Klabu zote mbili zilifikia muafaka wa kuuziana golikipa huyo lakini uhamisho huo ulikwama kutokana na kufikia muda wa mwisho wa usajili huku De Gea sasa akilazimika kubakia United mpaka Januari mwakani wakati dirisha dogo litakapofunguliwa. Akihojiwa Perez amesema De Gea alikuwa yuko tayari kwa uhamisho na anachoshindwa kuelewa ni kwanini United walisubiri mpaka siku ya mwisho ndio wamuuze golikipa huyo. Rais huyo aliendelea kudai kuwa De Gea ameathirika kwa kiasi kikubwa kwasababu alikuwa anataka sana kujiunga na Madrid. Perez amesema walituma karatasi za mkataba mapema kabisa lakini anashangaa United kuchukua muda mrefu kurejesha karatasi hizo.

No comments:

Post a Comment