Friday, September 4, 2015

WELBECK KUREJEA DESEMBA.

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Danny Welbeck anatarajiwa kukaa nje ya uwanja mpaka Desemba mwaka huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti. Klabu hiyo ilifafanua kuwa matibabu ya goti ya nyota huyo hayakwenda vizuri na wiki iliyopita hivyo ikaamuliwa afanyiwe operesheni. Welbeck, aliumia goti lake Aprili huku akiwa kaifungi timu yake ya Arsenal mabao 8 katika mechi 34 alizocheza toka atue Emirates akitokea Manchester United. Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal ambayo haikusajili mshambuliaji dirisha la usajili la kiangazi lililofungwa juzi. Mfaransa Oliver Giroud anabaki kuwa mshambuliaji pekee wa kutumainiwa katika kikosi hicho.

No comments:

Post a Comment