SHIRIKISHO la Soka nchini-TFF, limelishitaki Shirikisho la Soka la Nigeria-NFF kwa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF wakiwatuhumu kushindwa kutoa ushirikiano. Katika barua hiyo nzito kwa CAF, TFF imejitoa kushughulika na kitu chochote kinachohusu timu ya taifa ya Nigeria wakati wakiwa hapa Tanzania. Akizungumza na mtandao wa Supersport.com, rais wa TFF Jamal Malinzi amewatuhumu NFF kuwaacha gizani na kutojua chochote kinachoendelea tofautia na utaratibu unavyotaka. Malinzi amesema wamesikitisha na hatua ya NFF ambayo imeonyesha kuwakosea heshima kwani wameshindwa kuwataarifu ujio wao na hata hoteli waliyofikia wamefanya kuwa siri. Rais huyo aliendelea kudai kuwa wamechukulia suala hilo kama kitu kisicho kizuri kwani wao ndio wenyeji wao halafu hawafamu lolote kuhusiana na wageni wao. Malinzi amesema kufanya hivyo ni kujiweka wenyewe katika hatari kwani hawawezi kuwaandalia chochote hata usafiri wa ndani kwani hawawapi ushirikiano wowote ndio maana wameamua kuitaarifu CAF ili likitokea lakuja kutokea baadae wasipewe lawama wao. Nigeria waliingia jana jioni tayari kwa ajili ya mchezo huo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2017 dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars unaotarajiwa kuchezwa kesho jioni katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment