Tuesday, September 1, 2015

LESCOTT KWENDA VILLA.

BEKI Joleon Lescott amekamilisha vipimo vya afya katika klabu ya Aston Villa kabla ya kukamilisha uhamisho wake kutoka kwa West Bromwich Albion. Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 32 anetegemewa kukamilisha rasmi uhamisho wake leo kwa ada inayotarajiwa kufikia paundi milioni mbili. Lescott ambaye ameichezea Uingereza mechi 2, alijiunga na West Brom Juni mwaka 2014 baada ya mkataba wake kuisha Manchester City. Beki huyo anaondoka West Brom baada ya ujio wa nyota John Evans aliyetoka Manchester United na James Chester kutoka Hull City.

No comments:

Post a Comment