Tuesday, September 1, 2015

MAN CITY YAMUACHIA DENAYER KWA MKOPO KWENDA GALATASARAY.

BEKI wa Manchester City, Jason Denayer amejiunga na klabu ya Galatasaray ya Uturuki kwa mkopo wa msimu mzima. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 20, ambaye alisaini mkataba wa miaka mitano, bado hajapata nafasi katika kikosi cha City baada ya msimu uliopita pia kucheza katika klabu ya Celtic. Akiwa Celtic, Denayer alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka anayechipukia na kuitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Ubelgiji Machi mwaka huu. Beki huyo sasa anaweza kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Galatasaray ambao wamepangwa kundi C sambamba na Benfica, Atletico Madrid na Astana.

No comments:

Post a Comment