MSHAMBULIAJI mkongwe Claudio Pizarro amejiunga tena na klabu ya Werder Bremen kwa mara ya tatu bada ya kukubali mkataba wa kuitumikia mpaka mwishoni mwa msimu huu. Mkongwe huyo kwa mara ya kwanza aliiwakilisha klabu hiyo ya Bundesliga kati ya mwaka 1999 na 2001 kabla ya kuondoka na kwenda kujiunga na Bayern Munich. Pizarro alirejea tena Bremen kwa mkopo Agosti mwaka 2008 kufuatia kuchindwa kung’aa katika Ligi Kuu akiwa na chelsea kabla ya kusaini mkataba wa moja kwa moja mwaka mmoja baadae. Mkongwe huyo wa kimataifa wa Peru aliondoka tena Bremen kwenda bayern msimu wa 2012-2013 lakini mkataba wake na mabingwa hao wa Bundesliga hakuongezwa hivyo kumfanya kuondoka kama mchezaji huru. Akihojiwa Pizarro amesema amefurahishwa kurejea tena Bremen anategemea kukutana na changamoto lakini ni matumaini yake atautumia uzoefu wake kuisadia klabu hiyo kusonga mbele.
No comments:
Post a Comment