KOCHA wa timu ya taifa ya Wales, Chris Coleman ana uhakika wa kufuzu michuano ya Euro 2016 pamoja na kulazimishwa sare ya bila kufungana na Israel katika mchezo uliofanyika huko Cardiff. Ushindi katika mchezo huo ungewahakikishia nafasi kufuzu Wales na kuondoa ukame wa kutoshiriki michuano mikubwa toka mwaka 1958, huku wakiwa wamebaki na michezo miwili mkononi. Hata hivyo, Wales sasa wanahitaji alama moja katika mchezo wao wa ugenini dhidi ya Bosnia-Herzegovina utakaofanyika Octoba 10 au wakikosa huko wapate alama hiyo kutoka kwa wanyoke katika kundi lao Andorra ambao watacheza nao Octoba 13. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Coleman amesema imewahuzunisha kidogo kushindwa kupata alama tatu muhimu walizohitaji katika mchezo huo lakini jambo hilo halijawakatisha tamaa kwani wana uhakika wa kujihakikishia nafasi hiyo katika mechi zinazofuata.
No comments:
Post a Comment