WACHEZAJI wawili nyota wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang na Lukasz Piszczek wote wamerejea klabuni mapema kutoka katika majukumu ya kimataifa kwasababu ya majeruhi. Aubameyang ambaye ni mshambuliaji wa kutumainiwa wa Gabon alipata majeruhi ya kifundo cha mguu katika mchezo ambao nchi yake iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Sudan katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2017 Jumamosi iliyopita. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye alifunga bao la nne katika mchezo huo aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiwaondoa hofu mashabiki wake kwa kudai kuwa majeruhi aliyopata sio makubwa sana na anaweza kucheza mchezo wa Bundesliga dhidi ya Hannover Jumamosi hii. Piszczek pia ana matumaini ya kuwepo katika kikosi cha Dortmund wikiendi hii, pamoja na majeruhi ya nyonga aliyopata wakati nchi Poland ilipotandikwa mabao 3-1 na Ujerumani katika mchezo wa kufuzu michuano ya Euro 2016 Ijumaa iliyopita.
No comments:
Post a Comment