Tuesday, October 6, 2015

AL AHLY YATIMUA KOCHA.

KLABU ya Al Ahly ya Misri imetimua kocha wake fathi Mabrouk baada ya wakongwe hao kushindwa kushinda taji lolote kubwa toka msimu wa 2003-2004. Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Alaa Abdel-Salek naye pia alitimuliwa kufuatia kikao cha bodi kilichokutana jana. Mchezaji wa zamani Abdel Aziz Abdel Shafi anayejulikana kama Zizo ndio amepewa mikoba ya kuinoa klabu hiyo kwa muda kwa mara ya pili. Mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa mwaka 2010 wakati alipotimuliwa Hossam Al Badry ingawa safari anapewa nafasi ya kupewa kazi moja kwa moja. Kilichochangia kwa kiasi kikubwa Mabrouk kutimuliwa ni kutolewa kwao katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Jumapili na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment