Tuesday, October 6, 2015

FERGUSON ASISITIZA KUFANYA UAMUZI SAHIHI KUMCHAGUA MOYES.

MENEJA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema hakufanya makosa kumchukua David Moyes kuchukua mikoba yake katika klabu hiyo. Ferguson ametetea uteuzi wa meneja huyo wa zamani wa Everton ambaye alitimuliwa baa da ya miezi nane, katika kipindi chake kipya kiitwacho siri ya mafanikio ambacho kinatarajiwa kuanza kurushwa Jumapili hii. Mkongwe huyo amesema walifanya kila wawezalo katika hali waliyokuwa nayo wakati huo na anadhani walichagua meneja sahihi pamoja na kwamba mambo hayakwenda kama yalivyotarajiwa. Ferguson amesema wakati ule Jose Mourinho alikuwa yuko njiani kurejea Chelsea, Carlo Ancelotti alikuwa anakwenda Real Madrid, Jurgen Klopp alikuwa amesaini mkataba mpya na Borussia Dortmund huku Louis van Gaal akisubiria michuano ya Kombe la Dunia. Kocha huyo aliongeza kuwa wakati ulikuwa hauko upande wao kupata meneja ambaye watu wengi walimuhitaji ingawa mpaka leo anaamini Moyes alikuwa sahihi kwa kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment