MENEJA wa Real Madrid, Rafa Benitez amesisitiza hana shaka na uamuzi wa Karim Benzema kuweka wazi kukerwa kwake na suala la kutolewa mara kwa mara, akimtaja mshambuliaji huo kama wa aina yake. Benzema aliwaambia wanahabari kuchukizwa na uamuzi wa meneja wake kumtoa kwa mara ya tano katika mechi sita alizoanza wakati walipopata sare ya bao 1-1 dhidi ya Atletico Madrid mwishoni mwa wiki iliyopita. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amesema amechoshwa na kutolewa kwake mara kwa mara ila atatulia na kuendelea kujituma ili asiwe akitolewa mara zote. Hata hivyo, Benitez amesema maneno ya Benzema hayajamsumbua kwani anampenda mshambuliaji huyo kutokana na ubora wake alionao. Benzema amefunga mabao saba katika mechi nane alizocheza msimu huu mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment