Monday, October 12, 2015

ALBANIA YAJIWEKEA HISTORIA EURO 2016.

TIMU ya taifa ya Albania jana imeweka historia mpya nchini kwao kufuatia kufuzu michuano ya Euro 2016, ikiwa ni mashindano ya kwanza makubwa kuwahi kushiriki. Albania ilipata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Armenia na kuwafanya kushika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi I juu ya Denmark na kuzua shangwe kubwa nchini humo. Ureno ambao walishinda mabao 2-1 ugenini dhidi ya Serbia ndio wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 21, wakifuatiwa na Albania wenye alama 14 na Denmark wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 12 wakisubiri hatua ya mtoano ili kujua hatma yao. Serbia na Armenia ambao ndio vibonde wa kundi hilo wamemaliza mechi zao za makundi wakiambulia alama mbili kila mmoja.

No comments:

Post a Comment